Monday, July 21, 2014

MAUMIVU YA KIFUA (CHEST PAIN)


 Kifua kuuma ni dalili ya magonjwa mengi sana, zaidi ya magonjwa 100 huweza kusababisha kifua kuuma.
 Lakini pia ni dalili ambayo haitakiwi kupuuzwa au kuchukuliwa kirahisi kwani inaweza kuwa dalili ya magonjwa hatari na yanayoweza kusababisha kupoteza maisha haraka – kama magonjwa ya moyo (heart attack) au ya mapafu (pulmonary embolism)
 Kutokana na umuhimu wa dalili hii, napenda tuangalie mambo machache ya muhimu kufahamu kuhusu maumivu ya kifua.

Angalizo: 

Usitumie ushauri na taarifa kutoka kwenye ukurasa huu kujichunguza au kujitibia mwenyewe nyumbani, Nenda kamuone daktari ili ufanyiwe uchunguzi sahihi na kutibiwa. Taarifa zilizoko kwenye ukurasa huu zikusaidie kutambua hatua za kuchukua upatapo na maumivu ya kifua au inapobidi kimsaidia mtu mwenye tatizo hilo.

MAGONJWA YASABABISHAYO KIFUA KUUMA NA DALILI ZAKE:

 

MAGONJWA YA MOYO:

 Mshituko wa moyo (Heart attack/ Angina Pectoris)
 Vijidudu kwenye moyo (infections) – (Pericarditis, myocarditis,endocarditis)
 Matatizo ya valve za moyo
 Magonjwa ya mshipa mkuu wa damu (aortic aneurysm, dissection)



Mshituko wa moyo(Heart Attack)
Dalili:
 Kifua kuuma kama mzigo mzito umekandamiza moyo
 Au maumivu makali kama mshale umekaa kwenye moyo
 Maumivu husikika upande wa kushoto wa kifua, sehemu ya katikati au yaweza kuwa popote kifuani
 Pia huweza kusikika kwenye bega, shingo, taya, mkono wa kushoto au hata kwenye meno (Radiating pain type).
 Kifua huwa kizito, na kujisikia kukosa hewa
 Moyo kuenda mbio
 Kutoka jasho jingi, kizunguzungu, kutapika au kwikwi isiyokatika
 Pia dalili nyingine huweza kujitokeza kama – kupoteza fahamu, tumbo kuuma n.k
 Maumivu huzidishwa na mishughuliko (activities/exertion) au msongo wa mawazo(stress). Kutulia au kupumzika (rest/relax) huleta nafuu au kuondoa maumivu.
 Homa hutokana na kuwepo kwa vijidudu (infection) kwenye moyo au damu.

MUHUMU: Ukipata dalili moja au zaidi kama zilizotajwa hapo juu, au maumivu ya kifua yasiyoisha zaidi ya dakika tano au yasiyotulia hata baada ya kupumzika au kutumia dawa za maumivu, tafadhali wahi hosipitali! Inapowezekana tafuta huduma ya matibabu ya haraka ya wagonjwa waliozidiwa(emergency care).




MAGONJWA YA KIFUA:

Damu kuvilia kwenye mapafu
(Pulmonary Embolism)
 Damu kuvilia kwenye mishipa ya damu ya mapafu (pulmonary embolism)
 Vijidudu kwenye mapafu – husababisha homa ya vichomi (Pneumonia, Bronchitis, Tuberculosis/TB,) n.k.
 Kujaa maji, damu au hewa kwenye mfuko wa nje wa mapafu (pneumothorax, haemothorax or pleura effusion)
 Saratani
Picha inayoonyesha damu iliyovilia kwenye mapafu (Pulmonary embolism)

Dalili:

 Haya husababisha maumivu ya kifua aina ya vichomi,
 Au maumivu makali wakati wa kupumua – kuvuta hewa
 Maumivu huwa popote katika kifua, bila kusikika nje ya kifua kama kwenye bega au shingo (non radiating type)
 Husababisha shida katika kupumua, mtu kujisikia kukosa hewa na kuhema haraka haraka
 Mara nyingine husababisha rangi ya midomo au mikono kubadilika kuwa blue(cyanosis)
 Homa au kutoka jasho sana hasa wakati wa usiku huashiria vijidudu – virusi, bacteria, TB nk.
 Mara nyingi huambatana na kikohozi – kikavu au chenye makohozi


MAGONJWA YA MFUMO WA CHAKULA:

 Kiungulia au Vidonda vya tumbo
 Michubuko au vijidudu kwenye njia ya chakula (oesophagitis)
 Magonjwa mengine ya njia ya chakula, tumbo, kongosho au hata ini.


Dalili:

 Husababisha maumivu ya kifua hasa sehemu ya chini, katikati ya matiti,
 Huweza kuwa kama moto, au maumivu tu makali katika eneo hilo
 Wakati mwingine husikika sehemu ya chini ya moyo upande wa kushoto
 Usambaaji wake(radiation) huelekea upande wa bega la kulia au mgongoni
 Mara nyingi huwa na uhusiano na chakula – maumivu wakati wa kumeza, baada ya kula, wakati mtu ana njaa, baada ya kula aina fulani ya vyakula, au akibadilisha utaratibu wa chakula.
 Kama tatizo limeshakuwa kubwa huweza kusababisha maumivu makali hata bila kuhusiana na chakula.

MAGONJWA YA NGOZI, MISULI NA MUFUPA YA KIFUA

 Moto wa mungu (Herpes zoster) kwenye eneo la kifua
 Magonjwa ya matiti
 Magonjwa ya mifupa au vishikizo vya uti wa mgongo
 Magonjwa ya mishipa ya fahamu ya kufua
 Michubuko, kuumia au kuvutika kwa misuli katika kifua
 Michubuko, vijidudu au kuumia mifupa, viungo(joints) au vishikizo vya viungo(tendons and ligaments) katika eneo la kifua
 Magonjwa mengine ya misuli na mifupa ya kifua

Dalili:

 Maumivu yanayosababishwa na magonjwa haya huweza kufana na maumivu yeyote yaliyotajwa hapo juu.
 Ni muhimu kujua historia au maelezo ya maumivu hayo kwa undani, kufanyiwa uchunguzi wa kina na vipimo pale vinapohitajika ili kujua tatizo.

MAGONJWA MENGINE NJE YA KIFUA YANAYOWEZA KUSABABISHA KIFUA KUUMA

 Magonjwa ya kisaikolojia au kuhema haraka karaka
 Sumu za aina fulani kama – lead, carbon monoxide
 Magonjwa ya Saratani


MUHIMU: 

Magonjwa yanayosababisha maumivu ya kifua, hasa yatokanayo na moyo au mapafu huweza kusababisha kupoteza maisha haraka sana kama yasipotibiwa kwa wakati. Tafadhali wahi hospitali ili upatiwe tiba mapema na kuokoa maisha yako. Usipuuzie maumivu ya kifua; Ni afadhali kumsumbua daktari kwa kuwahi hospitali na kukuta hakuna tatizo, kuliko kuogopa kumsumbua daktari halafu ukachelewa hospitali na kupata madhara ambayo yangeweza kuzuilika, au kupoteza maisha.

12 comments:

  1. Nimependa ushauri wako/wenu na maelezo ya kina kuhusu magonjwa ya kifua, Ahsante sana.

    ReplyDelete
  2. Asante kwa ushauri ila mimi pia ninatatizo la maumivu kwenye kifua .. Historia yangu hiko ivii kwa sasa nina miaka 25. mwanzoni nlikusina kabisa maumivu ya kifua ila Kuna wakati nkawa naenda fanya mazoezi gym .Mwendelezo wa gym kwa mala ya kwanza kama kawaida nikawa na maumivu ya kawaida na yakaisha nikawa kawaida ila pia kunawakat nikaacha kwenda gym kwa muda nkawa tuu nafanyaa mazoez ya kawaida mwenyewe ila tangia siku izo nmeanza mazoezi mpaka sasa nina maumivu makali kifuani . Kwa kipindi kingine nkifanya mazoezi kwa sana kinatulia na nilishawahi kwenda hospital nkafanya vipimo nkaambiwa sina titizo lolote so naombeni ushauri

    ReplyDelete
  3. Asente sana nimejifunza vitu vingi doctor

    ReplyDelete
  4. Bless you Dr. Are you also in socia media? Nawezaje kuwasiliana na wewe in person!?

    ReplyDelete
  5. hello doctor naumwa hayo maumivu mwez na nusu sasa naona yanazid kifua kinaniuma na katikat ya ziwa sijui nakupataje

    ReplyDelete
  6. nini huwa inasababisha mwili kuwa mzito na unashindwa mpaka kukimbia?

    ReplyDelete